IQNA

Haram ya Imam Ridha  (AS) kutoa huduma kwa lugha za kimataifa wakati wa ‘Wiki ya Karamat’

22:51 - April 19, 2025
Habari ID: 3480563
IQNA – Astan Quds Razavi, yaani  Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS) huko Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran, immepanga mfululizo wa programu za lugha mbalimbali kwa ajili ya wafanyaziara wa kimataifa wakati wa maadhimisho ya kuzaliwa kwa Imam Ridha (AS) wa nane wa Waislamu wa madhehebu ya Shia.

Akizungumza na IQNA, Hujjatul Islam Seyyed Mohammad Zolfaghari, Mkurugenzi wa Masuala ya Wafanyazaira wa Kigenikatika haram hiyo, amesema sherehe hizo zinalenga kuwajulisha wageni kutoka kote ulimwenguni juu ya urithi wa kiroho na kitamaduni wa Imam Ridha  (AS).

“Wiki ya Karamat ni fursa kwa wafanyaziara  kutoka kote ulimwenguni kuungana na mafundisho safi ya Imam Ridha (AS) na kufaidika na baraka za kiroho za siku hizi,” alisema.

Wiki ya Karamat huadhimishwa kuanzia tarehe 1 hadi 11 ya Dhu al-Qa'dah katika kalenda ya Kiislamu ya Hijria Qamaria, ikikumbuka siku za kuzaliwa kwa Bibi Maasuma (SA) na kaka yake ambaye ni Imam Ridha (AS). Neno “karamat” linamaanisha ukarimu au heshima, likiwa ni ishara ya sifa zinazohusishwa na Imam na dada yake. Wiki hii huadhimishwa kupitia shughuli mbalimbali za kitamaduni na kidini kote Iran.

Mwaka huu, kwa mujibu wa Zolfaghari, shughuli kuu kwa wageni wasio Wairani ni pamoja na vikao vya miongozo ya kiroho kwa lugha nyingi, mikusanyiko ya mashairi ya kidini, semina za kitamaduni, na mashindano ya kielimu.

Matukio maalum kwa wazungumzaji wa Kiarabu, Kihindi, Kiazeri, na Kiingereza ni pamoja na miduara ya Qur'ani, usimulizi wa hadithi kwa watoto, na maonyesho ya kisanii.

Kama ishara ya maelewano kati ya dini mbalimbali, maua pia yatatolewa kwa watalii wasio Waislamu.

“Programu hizi zinaonyesha umoja katika utofauti na ukarimu wa Imam wa nane,” Zolfaghari amesisitiza.

Matukio haya yanafanyika katika Haram ya Imam Ridha (AS), moja ya maeneo matakatifu zaidi katika madhehebu ya Shia.

3492741

Habari zinazohusiana
captcha